COURAGE

Description :

                           ☆Kwa kuwa Umeamua☆

USIKATE TAMAA

Maisha Yana changamoto nyingi sana, Kuna Wakati changamoto zinakuwa nyingi hadi unaonekana msumbufu na mzigo hadi rafiki zako wa karibu na ndugu nao hukuchukia na kukutenga kisa tu shida zimekuzidi hadi ukijikuna kichwani inatoka vumbi.
☆usilitazame kama vumbi hilo bali ni "catalyst "☆
Ya kwamba ukaze mwendo

Wapo baadhi ya rafiki zako ambao huenda uliwahi kusoma nao kwakuwa tu mambo yaliwaendea vyema wakapata ajira nzuri hawa nao hukutenga na huanzisha umoja wao na wakasapotiana kwa kila kitu lakini ikitokea siku mmekaa pamoja wewe ambaye maisha hayajakaa sawa hata ukitoa wazo hata Kama ni zuri watalipinga kisa tu wazo limetolewa na mtu asiye na hela.

Wapo marafiki zako ambao hata ukiwapigia simu hawawezi kupokea wataiangalia ikiita hadi kukata na wasikutafute huku wakikutukana kimoyomoyo kwamba "huyu mpumbavu ananipigia simu ananini? Au anajua mie benki) na baadhi ya maneno.

Wapo marafiki zako kisa hauna hela kwa wakati huo wao kila unachokifanya wataishia tu kusema "Yule!?, hafiki kokote Hana hela) wakati huo wakiwa bar kwenye viti virefu wapiga urabu na kuona maisha wameshayashinda.

Wapo marafiki zako pamoja na shida ulizonazo hata ukiwakuta maofisini hawawezi kukusaidia connection yoyote hata Kama wanaweza kufanya hivyo au lipo ndani ya uwezo wake yaani yupo radhi akuombe pesa kwa kisingizio cha bosi anataka hela ya chai ili tu akupige pesa na shida yako isifanikiwe.

Usikate tamaa endelea na kupambana na ukumbuke juhudi ulizo nazo ndio zitasaidia kukutoa sehemu moja kwenda nyingine, hali uliyo nayo either ya umasikini au kukosa ajira ni ya muda tu kuna lakini nakuhakikishia wakati wako ukifika hao hao waliokuwa wakikutenga na kukusengenya wataanza kurudi wenyewe na kukuita majina lukuki kama KIONGOZI, BOSS, MZEE BABA wakati zamani walikubatiza kila jina lililo baya kwako; ☆Hao ni wanafiki, usiwazingatie, wajibu majibu ya kawaida tena kwa wema kabisa..☆

na hapa ndipo inapokuja dhana ya kwamba "mshukuru Mungu kwa kila jumbo " maana wakati wako ukifika hutenda miujiza isiyo ya kubahatisha.

Terms & conditions :

Related Services

This site was designed with Websites.co.in - Website Builder

IMPORTANT NOTICE
DISCLAIMER

This website was created by a user of Websites.co.in, a free instant website builder. Websites.co.in does NOT endorse, verify, or guarantee the accuracy, safety, or legality of this site's content, products, or services. Always exercise caution—do not share sensitive data or make payments without independent verification. Report suspicious activity by clicking the report abuse below.

WhatsApp Google Map

Safety and Abuse Reporting

Thanks for being awesome!

We appreciate you contacting us. Our support will get back in touch with you soon!

Have a great day!

Are you sure you want to report abuse against this website?

Please note that your query will be processed only if we find it relevant. Rest all requests will be ignored. If you need help with the website, please login to your dashboard and connect to support

;